• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mara yaazimia kufuatilia utekelezaji wa miradi ya barabara

Posted on: January 6th, 2026

Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara iliyofanya kikao chake cha kawaida kilichofanyika leo tarehe 06 Januari, 2026 kimeazimia kuzifuatilia mamlaka zinazohusika ili wakandarasi waliotekeleza miradi ya barabara wanaodai fedha walipwe ili waweze kuendelea kutengeneza barabara za Mkoa wa Mara.

Maazimio mengine ni fedha zilizotengwa kwenye bajeti kwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya Barabara Mkoa wa Mara zitolewe ili miradi iendelee kutekelezwa; kuharakishwa kwa zabuni ya miradi ya barabara zikamilishwe haraka ili wakandarasi waweze kupatikana na kutekeleza miradi ya barabara kwa haraka.

“Hali ya barabara katika Wilaya za Serengeti na Rorya ni mbaya zaidi kwani wilaya hizi hazijaunganishwa kwa barabara ya lami na Mkoa au hata kutoka makao makuu ya wilaya hizo na wilaya nyingine zinazozunguka wilaya hizo” amesema Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi ambaye ni Mwenyekiti wa kikao hicho. 

Mhe. Mtambi pia amewataka wabunge na madiwani wa Mkoa wa Mara kufanyakazi kama timu moja na kupata taarifa rasmi za hali ya barabara kutoka kwa taasisi za husika za umma ili viongozi wote wa Mkoa wa Mara waongee lugha moja wanapofuatilia utejekezaji wa miradi katika mamlaka mbalimbali za Serikali.

Aidha, Bodi hiyo imeazimia kuishauri Serikali kupitia Shirika la Hifadhi ya Wanyamapori (TANAPA) kufanya matengenezo ya barabara ya mara kwa mara ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) na kutengeneza barabara mbadala za kudumu katika hifadhi hiyo ili kuwahudumia watalii na wananchi wa Mkoa wa Mara. 

Kwa upande wake, Mbunge wa Bunda Mhe. Ester Bulaya amesema Hifadhi ya Taifa ya Serengeti baada ya kutangazwa kuwa hifadhi bora duniani na World Travel Awards, kwa miaka kadhaa mfulilizo anaamini idadi ya watalii kutoka ndani na nje ya nchi katika hifadhi hiyo itaongezeka jambo ambalo amesema litahitaji barabara imara zinazopitika wakati wote.

Mhe. Bulaya ameishaishauri Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara kuwasilisha ombi la dharura kwa Serikali kukarabati na kutengeneza barabara za kudumu katika hifadhi hiyo kwa haraka ili kuwahudumia watalii wanaotarajiwa kuongezeka katika hifadhi hiyo.

“Tunatarajia kupata watalii wengi ambao barabara zikiwa mbaya wanaweza kuanza kulalamika na watalii wakilalamika itapunguza idadi ya watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti” amesema Mhe. Bulaya.

Mhe. Bulaya ameeleza kuwa kwa sasa Hifadhi hiyo inahudumia magari zaidi ya 600 kwa siku na wingi wa magari hayo yanaendelea kuharibu barabara hizo jambo ambalo bila uwekezaji thabiti linaweza kuleta malalamiko ya ubovu wa barabara.  

Akiwasilisha taarifa ya Wakala wa Barabara (TANROADS) Meneja wa Mkoa wa Mara Mhandisi Ezra Magogo Daniel amesema TARNROADS Mkoa wa Mara inahudumia barabara zenye urefu wa kilomita 1,449.65 ambapo kati yake barabara kuu ni kilomita 409.73; barabara za Mkoa ni kilomita 976.54; na barabara zilizokasimiwa kilomita 63.38.

Mhandisi Daniel amesema kutokana na tathmini ya barabara iliyofanyika Septemba, 2025 kilomita 528.82 ambayo ni sawa na asilimia 36.5 ya barabara zote za Mkoa wa Mara zipo katika hali nzuri; kilomita 869.13 sawa na asilimia 60 ni wastani wakati kilomita 51.7 sawa na asilimia 3.5 zipo katika hali mbaya.

Mhandisi Daniel amesema sehemu kubwa ya barabara zilizo katika hali mbaya inatokana na barabara zilizomo kwenye miradi ya kitaifa ambayo ujenzi wake unaendelea na ujenzi huo ukikamilika Mkoa wa Mara utakuwa umepunguza kilomita za barabara zilizo katika hali mbaya.

Aidha, Mhandisi Daniel ametoa taarifa za uwepo wa mizani katika maeneo ya Sirari (Tarime), Rubana na Nyantare (Bunda) ambayo amesema imeendelea kupima magari na kulipisha faini kwa magari yaliyozidisha uzito wa mizigo kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake, Meneja wa TARURA Mkoa wa Mara Mhandisi William Lameck amesema TARURA Mkoa wa Mara ina mtandao wa barabara zenye urefu wa kilomita 4,559.08 na kulingana na tathmini iliyofanywa Juni, 2025 asilimia 52.93 upo katika hali nzuri; asilimia 28.32 ni wastani wakati asilimia 18.75 zina hali mbaya.

“Kwa wastani zaidi ya asilimia 80 ya barabara zote zinazohudumiwa na TARURA katika Mkoa wa Mara zinapitika mwaka mzima isipokuwa kwenye maeneo machache ambayo ni korofi” amesema Mhandisi Lameck.

 Kikao hicho kimehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mara, Kamati ya Usalama ya Mkoa, wabunge, Meya, Wenyeviti na wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mara, Maafisa kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara na Mkoa wa Kipolisi wa Tarime Rorya, TARURA, TANROADS, SENAPA, TEMESA na LATRA.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Mtambi kuwaongoza watumishi mazishi ya Saaban Ndalu

    January 30, 2026
  • TISEZA yazindua dawati la uwekezaji Mara

    January 27, 2026
  • TISEZA yahamasisha uwekezaji katika fursa za Mkoa wa Mara

    January 24, 2026
  • Mtambi afanya ziara Butiama

    January 20, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa